Kikosi cha wawakilishi watanzania katika michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga wamewasili salama nchini Algerai kwa ajili ya mchezo wao marudiano dhidi ya MC Alger utakaochezwa kesho majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Katika msafara huo uliiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa umefika salama na ukipokelewa na watanzania wanaoishi nchi Algeria na kufurahishwa na mapokezi hayo na kuahidi ushindi kwa watanzania.
Msafara wa wachezaji hao uliingia kwa mafungu mawili ambapo kundi la kwanza liliwasili likiongozwa na benchi la ufundi la timu hiyo likiwa na kocha Mkuu George Lwandamina huku kurudi la pili likiwasili  na Katibu Mkuu.
Mtanzania Hamis Mwampese anayeishi nchini Algeria amesema kuwa timu ya Algers wameingia uoga hasa baada ya kuona Yanga wamechelewa kuingia nchini humo na zaidi kwa kufanya hivyo wameepusha sana kufanyiwa hujuma na wenyeji wa nchi hiyo.
Yanga wamefikia katika Hotel ya nyota tano inayojulikana kwa jina la Sultan ambapo si mbali sana na Uwanja ulipo utakaochezewa kesho katika mechi hiyo ya marudiano ambapo Yanga wanatakiwa kupata ushindi wa aina yoyote au sare.

Mtanzania Hamis Mwampese akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa baada ya kuwasili Jijini Algeria  kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mc Alger ambapo katika mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa goli 1-0..

Mtanzania Hamis Mwampese  akiwa katika picha mbalimbali na wachezaji wa timu hiyo baada ya kuwasili nchini Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mc Alger ambapo katika mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa goli 1-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...