Wateja watakaojaza mafuta ya magari kuanzia shilingi 50,000 na kuendelea kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya ENGEN nchini kote kuanzia leo na kulipia kupitia huduma ya Lipa kwa M-Pesa ya Vodacom Tanzania Plc watajipatia ofa papo hapo ya mafuta ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/-.

Wateja watakaojaza mafuta ya magari kuanzia shilingi 50,000 na kuendelea kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya ENGEN nchini kote kuanzia leo na kulipia kupitia huduma ya Lipa kwa M-Pesa ya Vodacom Tanzania Plc watajipatia ofa papo hapo ya mafuta ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/-.

Ofa hii inatokana na kampeni ya Vodacom Tanzania Plc inayohamasisha wananchi kuacha utaratibu wa kutumia fedha taslimu wanapofanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali badala yake watumie huduma ya Lipa kwa M-Pesa ambayo hivi sasa imerahisishwa zaidi na mtandao huo kuwa salama katika masuala ya kibiashara.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii, Mkurugenzi wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit alisema “Huduma ya Lipa kwa M-Pesa imeboreshwa zaidi; mbali na kuwawezesha wateja kulipa bila makato yoyote, malipo yamerahishwa zaidi kupitia M-PESA APP mpya yenye teknolojia ya QR codes na wateja wa Vodacom watazawadiwa dakika za BURE kila wanapolipa. Kizuri zaidi ni kwamba sasa wateja wa mitandao mingine pia wanaweza kuwalipa wafanyabiashara waliosajiliwa na huduma hii moja kwa moja kutoka kwenye akaunti za simu za mitandao yao au akanti za benki’.

Alisema kampeni hii inaambatana na ofa mbalimbali kwa sekta tofauti kama ambavyo wateja watakaonunua mafuta kwenye vituo vya ENGEN watakavyozawadia mafuta BURE kila wanapolipia kwa M-PESA. Aliwashauri wateja kupakua APP mpya ya M-Pesa inayorahisha malipo Kwa kwenda Google Playstore na kutafuta ‘MPESA TANZANIA’ kisha wajionee urahisi wa kulipa kwa QR codes kwenye vituo vya ENGEN na maeneo mbalimbali.

“Natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kuachana na utamaduni wa kubeba mabulungutu ya fedha wanapotaka kununua bidhaa badala yake waweke fedha kwenye simu zao na kulipia kutumia kupitia M-Pesa, njia rahisi na salama inayorahisisha maisha kwa wateja na wafanyabiashara.Tunandelea na kampeni itakayofanyika nchini kote kuwaelimisha wananchi sambamba na kuwezesha wafanyabishara wengi zaidi kupokea malipo kwa M-Pesa’’. Alisema Sitoyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Engen Tanzania,Paul Muhato alisema “Wakati tunaendelea na wiki ya huduma kwa wateja kwa wateja wetu ambapo tunafanya shughuli mbalimbali, tunayo furaha kushirikiana na Vodacom katika kuhamasisha wananchi matumizi ya njia za kupata huduma bila kutumia fedha taslimu kama hii ya Malipo kwa M-Pesa njia ambayo ni rahisi na salama kwa watoa huduma na  wapata huduma.”

Alisema, Engen Tanzania ikiwa moja ya kampuni inayoongoza kutoa huduma za kuuza mafuta nchini itaendelea kuwaletea ubunifu wa huduma bora wateja wake na kuwapatia ofa mbalimbali kama ambavyo inawaletea ofa hii maalumu ya kupata mafuta ya bure kwa kushirikiana na Vodacom na lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wateja wetu wanaishi maisha ya kisasa kupitia mapinduzi ya kiteknolojia.

Mbali na ENGEN, huduma ya lipa kwa M-Pesa imeendelea kupokelewa vizuri na wafanyabiashara wengine kutoka sekta mbalimbali kama mahoteli na migahawa, bar na clubs, maduka ya rejereja, maduka ya madawa, maduka ya vifaa vya ujenzi, saluni n.k
Mkurugenzi wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit(kushoto) Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Engen,Mikocheni jijini Dar es Salaam,Abdalah Shomari, wakimshuhudia Mkurugenzi mtendaji wa Engen Tanzania,Paul Muhato akijaza mafuta kwenye gari la mteja baada ya kulipia kwa huduma ya Lipa kwa M-Pesa na kujipatia ofa ya mafuta ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/-wakati wa Uzinduzi wa ofa hiyo leo.
Mkurugenzi wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit(katikati)akijadiliana jambo na Mkurugenzi mtendaji wa Engen Tanzania,Paul Muhato(kulia)wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Lipa kwa M-Pesa kwa wateja watakaojaza mafuta ya magari kuanzia shilingi 50,000 na kuendelea kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya ENGEN nchini kote kuanzia leo na kujipatia ofa ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/- anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania PLC,Noel Mazoya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...