Katika kuleta ufanisi na ubunifu kwenye sekta ya Mawasiliano, ambayo imeleta mabadiliko kwenye maisha ya mamilioni ya Watanzania, Kampuni ya mawasiliano Zantel imeendelea kuboresha huduma za kisasa za mtandao wake ili kuhakikisha wateja wao wanazidi kufurahia huduma ya mtandao wenye kasi wa 4G.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Mchakato wa kuboresha mtandao wa Zantel visiwani Zanzibar na Tanzania Bara umekua ukiendelea vizuri, kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia manufaa ya teknolojia ya simu kupitia mtandao wa simu wa Zantel.”

Uboreshaji unaoendelea utaweza kuhimarisha zaidi ubora wa mtandao wetu, huduma za intaneti za kasi zinazotumiwa zaidi kwa sasa sokoni na wateja ni hii ya 4G.”

Aidha, aliongeza kwa kusema, Uboreshaji wa maeneo yote ya Stone Town na mikoa ya Magharibi umefanikiwa. Zoezi la kuendelea kuboresha huduma hizo kwa visiwa vya Unguja na Pemba linaendelea na litakamilika ifikapo Mei mwaka huu.

Mradi mzima utagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 hadi kukamilika. Mtandao wa Zantel utaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake, pamoja na mtandao utakaowafikia zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania wanaotumia huduma za simu ya mkononi zenye ubora zaidi, intaneti yenye kasi pamoja na kuboresha huduma za fedha.

Amesema mradi una lengo kufanya mabadiliko kwenye vituo vyote vya huduma za katika mitandao ya simu kwa kisiwa cha Zanzibar na Tanzania Bara kwa kufunga vifaa bora vya kisasa.

Mtandao wa Zantel unawakaribisha Watanzania wote kutumia na kufurahia huduma ya intarneti ya 4G kutoka Zantel kama kampuni ya mtandao wa simu ya kwanza kuleta huduma za kibenki kwa jamii ya Kiislamu na kwa nchi nzima.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulipita jijini Dar es salam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...