Na Ramadhani Ali-Maelezo

Taasisi zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na ukimwi Zanzibar zimetakiwa kuelekeza nguvu katika makundi maalum ambayo maambukizi bado ni makubwa.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alitoa ushauri hao alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa mapambano ya ukimwi uliotayarishwa na Taasisi ya kuimarisha huduma za afya Tanzania (THPS) na kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano wa taasisi hiyo katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.

Alisema wakati Zanzibar inajivunia kuwa na asilimia chini ya moja ya maambukizi ya VVU, katika makundi maalumu maamukizi yapo kwa asilimia 10 hadi 19 ambapo ni hatari.

Aliyataja makundi hayo kuwa ni vijana wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya, wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua mkutano wa wadau wa mapambano ya ukimwi Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizindua Mpango Mkakati wa miaka mitano wa THPS katika mkutano wa wadau wa mapambano ya ukimwi uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni, anaeshirikiana nae katika uzinduzi huo ni Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Redempta Mbatia.
Mkurugenzi Mtendaji wa THPS Dkt. Redempta Mbatia akizungumza na wadau wa mapambano ya ukimwi Zanzibar katika mkutano wa siku moja uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Muhudumu Mkuu wa huduma za mama na mtoto na huduma za upimaji vvu kwa jamii kutoka Hospitali ya Mwembeladu Mwanakhamis Alawi Nguzo akipokea zawadi maalum kutoka Waziri wa afya Mh. Thabit Kombo baada ya kuwa kituo bora katika mapambano ya ukimwi kipindi cha miezi mitatu Octoba – Disemba.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...