Mwanamuziki nyota wa kizazi kipya nchini, Ben Paul atatumbuiza katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (Miss Ustawi) yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini.

Mratibu wa mashindano hayo, Catherine Boniface alisema kuwa Paul ambaye anatamba na wimbo wa Moyo Machine, Phone na nyinginezo nyingi, pia atatambulisha wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanamuziki nyota nchini, Darasa.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na kinywaji cha Windhoek, yatashirikisha jumla ya warembo 12 ambao walikaa kambini kwa muda wa wiki mbili wakijifua chini ya mwalimu wao, Clara Michael na matron, Catherine Boniface.

Warembo ambao wamepitishwa na kamati ya mashindano hayo ni Fatma Kivea, Elice Mwakajila, Melody Thomas, Diana Mwaibula, Hapifania Shedoekulu, Careen Kileo. Wengine ni Angelina Michael, Ruth Deogratius, Consolator Samwel, Loyce Jeck na Elizabeth Julius.

Rais wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Yohana Mabena akizungumza wakati wa  kuwatambulisha warembo wao kwa wadhamini wakuu, kampuni ya Mabibo Beer. Kulia ni msemaji wa kampuni ya Mabibo Beer, Andrea Missama na kushoto kwa Mabena ni Waziri wa Michezo wa Ustawi, Ashura Jingu. Nyuma ni warembo wa miss Ustawi 2017. 
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Paul akizungumza akizungumza wakati wa kutambulishwa kuwa msanii wa kutumbuiza katika mashindano Miss Ustawi 2017 yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, jijini.

Miss Ustawi anayemaliza muda wake Evelyn Andrew akizungumza wakati wa utambulisho wa warembo hao kwa wadhamini wakuu. Evelyn anavua taji hilo, Ijumaa (Mei 19) wakati wa mashindano ya kumsaka mrembo wa chuo hicho kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...