Bank ya biashara Africa CBA imeanzisha huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa Bank hiyo Gift Shoko alisema lengo la kianzisha huduma hiyo ni kutoa fursa kwa watu wote kuchangia pato la taifa.

"Hivi sasa kuna watu wanakosa muda wa kwenda Bank kupanga foleni kutokana na majukumu mbalimbali, hivyo kuwepo kwa huduma hii kutawarahisishia kupata huduma bila kwenda Bank" alisema Shoko na kuongeza

"Ni fursa kwa taasisi na mashirika mbali mbali kuchangamkia huduma hii kwani itaambatana na kuduma kama kupewa vyumba vya kufanyia mikutano, kupewa msaada wa kisheria, kupata matibabu ya nje ya nchi na mteja kupewa mtu maalimu wa kumhudumia"

Kwa upande wake Solomon Kawiche mkuu wa kitengo cha masoko CBA alisema huduma hiyo itakuwa kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar es salaam licha ya kuwa na matawi Mbeya, Kigoma, Mtwara, Moshi na Tunduma.

Bank hiyo iliyoanza miaka ya 60 ambayo ipo Tanzania, Kenya na Uganda, yenye makao makuu mjini Nairobi hivi karibuni inatarajia kuanzaisha tawi Ivory cost kwa lengo la kujitanua zaidi kibiashara.
Mkurugenzi wa Bank ya biashara Africa CBA Gift Shoko akizungumza hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank(Habari Picha na Pamela Mollel blog)
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CBA N.Kitomari akizungumza katika uzinduzi huo hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank 
Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi katika benki ya CBA akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa hudum mpya kwa wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank .
Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi akimkabidhi zawadi moja ya wateja wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma mpya ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...