Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Insurance Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa bima ya Afya kwa wagonjwa wanaolazwa ambayo ni maalum kwa Wafanyakazi wa makampuni Makubwa, ya Kati na Madogo, katika Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Bima ya Afya wa Britam Insurance Tanzania, Christine Mwangi (wa pili kulia) akielezea namna Bima hiyo itakavyokuwa inafanya kazi kwa wateja wawatakaojinga na faida zake, wakati wa Mkutano na waandishi wa habari habari (hawapo pichani) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam. wengine pichani toka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala, Irene Godson, Afisa Mtendaji Mkuu Britam Insurance Tanzania, Stephen Lokonyo, Meneja wa Mauzo, Godfrey Mzee pamoja na Afisa Oparesheni, Farai Dogo. Picha na Othman Michuzi.
 Meneja wa Mauzo wa Britam Insurance Tanzania, Godfrey Mzee akizungumza.

Na Karama Kenyunko, 
Kampuni ya Bima ya Britam, imezindua huduma ya afya kwa makampuni ili kuwawezesha waajiri kupunguza garama pindi mfanyakazi anapolazwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam, Stephen Lokonyo, amesema bima hiyo itawapunguzia wananchi garama kubwa zitokanazo na kulazwa.

"Huduma hii inalenga wakati mtu anapopata matatizo makubwa, ndio maana tunelenga pale mtu unapougua na kulazwa hospitali" amesema Lokonyo.

Ameongeza kuwa, makampuni mengi yanapenda kutengeneza faida na siyo hasara hivyo. Bima ya Britam itamsaidia mwajiri kukwepa garama kubwa, ambayo kampuni inaweza kutumia kumtibu, mfanyakazi pindi anapolazwa, kwani anaweza akaumwa akashindwa kwenda kazini na kushindwa kufanya uzalishaji kazini lakini wakati huo huo kampuni inakuwa inamlipia matibabu.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wameisha saini mkataba na hospitali zaidi ya kumi nchini kama vile Aghakan, Hindumandal, Tumaini, Kairuki na zinginezo.

Naye Meneja Bima ya afya ya Britam Christine Mwangi ameongezea kuwa, watahakikisha makampuni yote ambayo yanaingia mkataba na huduma ya bima ya Britam watapatiwa huduma nzuri, kwani wameishafanya uchunguzi na kuweka mikakati yao sawa kuhakikisha kila mgonjwa anapatiwa huduma bora.
"Wakati mwingi kampuni za bima zinaingiza bidhaa bila kuelewa soko vizuri, lakini sisi tulichukua muda na kugundua kuwa haja kubwa katika bima ya afya ni kugaramia matibabu yatokanayo na kulazwa, sababu garama za matibabu madogo unaweza kugaramia mwenyewe lakini garama za kulazwa ni kubwa sana ndio maana tukaanzisha bima hii ya afya ya kulazwa." amesema Mwangi


Amesema, katika huduma hiyo, wagonjwa wataweza kutibiwa katika hospitali mbali mbali nchini na hata nje ya nchi, kama vile India, South Africa, Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...