Spika
wa Bunge Job Ndugai akimkabidhi kikombe Naodha wa timu ya Bunge Sports
Club ambaye ni Mbunge wa Mbiga, Sixtus Mapunda baada ya timu hiyo
kuifunga NMB Magori 2-0 wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye
Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Timu
ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa pete
ambaye iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19 kwa 2, ikifuatiwa na timu
ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya
mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37 kwa 28.
Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu ambayo iliwafunga NMB goli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.
Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana zikicheza michezo mbalimbali ikiwa na lengo ya kuboresha uhusiano baina ya Bunge na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo makao makuu ya nchi, Dodoma.

Abdulmajid
Nsekela- Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na wa kati NMB
akisalimiana na mchezaji wa Bunge Sports Club mpira wa Pete ambaye ni
Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kabla ya mchezo wa kirafiki wa Pete kati
ya Bunge na NMB.TIMU ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa
miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe
vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya Benki
za NMB.
Meneja
wa Kanda ya Kati wa NMB, Straton Chilongala akimkabidhi nahodha wa
mpira wa Pete wa Bunge Sports Club ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Esther
Matiko.
Abdulmajid Nsekela akikabidhi kikombe cha mpira wa Kikapu kwa washindi Bunge Sports Club.
Wachezaji
wa Bunge Sports Club na NMB mpira wa pete wakiwania mpira wakati wa
mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...