THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

FEMINA HIP YAJA NA KAMPENI MPYA YA NGUVU YA BINTI

Na  Ashraf Said, Globu ya jamii.

Tasisi ya Femina Hip imeanzisha kampeni yake mpya inayokwenda kwa jina la Nguvu ya Binti ili kumsaidia msichana anapokuwa katika siku zake .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Lydia Charles amesema kuwa Femina Hip imezindua kampeni ya Nguvu ya Binti ambayo itawakilishwa na wasichana wenye historia,Tabia, na uzoefu tofauti .

“ timu mpya ya nguvu ya binti itakuwa na sauti ya wasichana wote nchini Tanzania , wakichimbua , Kujadili na kujaribu kutatua changamoto na vikwazo mbalimbali kwa pamoja” amesema.
Amesema kuwa wasichana hao watakuwa mawakili kwa mambo ya kijamii, Kiuchumi na kisiasa.
Ameliza kwa kusema kuwa Femina Hip pamoja na wasichana wa kundi hilo wanamini kwamba ni lazima kufanya kazi pamoja , kufunguka na kuzungumza kuhusiana na hedhi ,maumivu wakati wa hedhi , Usafi wa miiko inayousishwa na hedhi kwa kushirikisha walimu , wazazi, walezi na Wanaume pia .
 Mratibu wa programu ya Nguvu ya Binti , Lydia Charles akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mpango wao wa kuwawezesha wanawake wanapokuwa katika siku zao leo katika ofisi zao  katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Kays Hygien, Sauda Simba akizungumzia kuhusu kampuni  ya Femina  iliyodhamini programu hiyo
Sehemu ya Waandishi wa wakufuatilia mkutano