Prof. John Lupala, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka wanachi kuzingatia Sheria Na. 8 ya mwaka 2007 kuepuka adha zinazotokana na kutozingatia sheria hiyo.

Akitoa ufafanuzi wa Sheria ya Mipango Miji, namba 8 ya mwaka 2007; Prof. Lupala alisema; Sheria imetungwa ili kutoa muongozo namna ya kupanga miji nchini. Prof. Lupala amefafanua maeneo matatu ya Mipango katika sheria hiyo. 

Mipango Kabambe/ General Planning; Mipango ambayo huandaliwa kuongoza ukuaji wa miji kwa muda wa miaka 20. Ambapo sheria inasisitiza ushiriki wa maoni ya Wananchi.

Mipango Kina; Mgawanyo wa viwanja au shamba unaofanywa katika eneo fulani, hutakiwa kuandaliwa kulingana na taratibu za viwango vya upangaji ndani ya miji, alieleza hata kama mpangaji binafsi anatumika ni lazima viwango vya kisheria vizingatiwe.

Urasimishaji; Unalenga kutambua miliki za watu, kutengeneza viwanja vya milki za maeneo yao na kupangilia miji kwa kuweka huduma za msingi au miundombinu ya msingi kama; maji, barabara n.k.

Pro.Lupala alisema iwapo mwananchi hatazingatia taratibu za uendelezaji Miji bila kupata kibali cha ujenzi, Mamlaka za Miji huchukua hatua kwa Kusimamisha ujenzi au kubomoa.

Wananchi hawana budi kushiriki katika maoni wakati wa upangaji miji na kutojenga katika maeneo hatarishi, ya hifadhi au oevu.


Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Prof. John Lupala akitoa ufafanuzi wa Sheria ya Mipango Miji, Na. 8 ya Mwaka 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...