Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji,Imezinduliwa rasmi na Vodacom Tanzania PLC jana,Huduma hiyo  inayojulikana kama“Ukarimu wa Vodacom” ni huduma ambayo ni muhimu kwa wateja wa kampuni hiyo katika kipindi hichi cha mwezi mutukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku. Vodacom imepata uzito wa kipekee kwa kuileta huduma hii haswa ususani kwa jamii za Pwani ambako kuna Waislamu wengi na kuwakumbusha kuendeleza mshikamano.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao anasema “Tumekusanya maoni mbalimbali ya kutosha kutoka sokoni ili kuweza kuelewa ni nini hasua jamii inahitaji. Tulifikiri sana ni nini tunaweza kufanya ambacho kingeweza kuwa mahsusi katika kipindi hiki, timu yangu iliona kampeni ni muhimu ikalenga kutoa kwa jamii
Walengwa wa kampeni hii ni jamii yetu pamoja na sifa zake za kuvutia, kampeni hii itaongeza thamani katika sifa hizo kupitia ukarimu, ushirika na utoaji chini ya kauli mbiu ya “Ukarimu wa Vodacom”
Kwa upande wake, Hendi Hisham ambaye ni mkurugenzi mkuu wa biashara wa kampuni hiyo anasema Tumefanya jitihada zote kuhakikisha kampeni hii inakuwa na mafanikio. Kampeni inahusu kurudisha kwa jamii za wateja wetu wa ukanda wa Pwani kwa Tanzania nzima,”
Alisema huduma hiyo itawezesha;
·        Kuziweka karibu zaidi familia na marafiki kutokana na dakika zaidi zitakazowawesha kupiga simu kipindi hikim cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kupitia Ukarimu wa Vodacom
·        Kwa kutambua umuhimu wa Ramadhan huduma hiyo itawapatia wateja huduma za bure kama vile mawaidha na kuwa kumbusha muda wa swala
·        Uwezo wa kupiga simu bure wakati wakisubiri kula “Daku”
·        Kugawa tende kwenye foleni bara barani ili kushiriki Ramadhan pamoja na jamii.

“Ili mteja aweza kunufaika na bando hili la Ukarimu anatakiwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba ,” anasema.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, bando hilo linampa mteja ujumbe mfupi wa maandishi wenye ujumbe wa dini ikiwamo hadithi, Qaswida, Dua, pamoja na Mwaidha kila siku bure.
“Faida nyingine ni pamoja na kupiga simu bure usiku kabla ya muda wa daku, Facebook na picha bure ” alieleza.
Alisema kwa shilingi 1000, mteja atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 10 kwenda mitandao yote, ujumbe mfupi wa maandishi wa maandhishi  bila kikomo, simu kupitia mtandao pamoja na ujumbe wa didi bure
Kwa mteja atakayenunua bando la shilingi 3000 atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 30 kwenda mitandao mingine, ujumbe mfupi wa maandishi bila kikomo, simu za bure usiku Vodacom kwenda  pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi wa dini bure kwa siku saba

 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kulia) kwenye uzinduzi wa kampeni ya Ukarimu wa Vodacom, wakati wa futali iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadjhan jijini Dar es Salaam jana.Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubery. Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji, itamwezesha mteja wa Vodacom Tanzania  kunufaika na bando hili la Ukarimu kwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba .
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizindua kampeni ya Ukarimu wa Vodacom  wakati wa futali iliyoandaliwa ya Vodacom Tanzania PLC  jijni Dar es Salaam jana Wanaoangalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa  kampuni hiyo, Ian Ferrao (katikati) na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubery. Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji, itamwezesha mteja wa Vodacom Tanzania kunufaika na bando hili la Ukarimu kwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba
Mkurugenzi Mkuu wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC, Hendi Hisham (kulia) akifafanua jambo kwa Mufti wa Tanzania Abubakary Zubery kwenye uzinduzi wa kampeni ya Ukarimu wa Vodacom, wakati wa futali iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam jana.Kampeni hiyo ilizinduliwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (katikati). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao. Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji, itamwezesha mteja wa Vodacom Tanzania kunufaika na bando hili la Ukarimu kwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...