Na. Benedict Liwenga-WHUSM, Moshi.

Kiwanda cha Utengenezaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC) iko mbioni kujenga mtambo utakaotumika katika kuyeyusha chuma kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake za utenegenezaji wa dhana mbalimbali za mashine ikiwemo kukarabati mifumo ya umeme ya kiwanda hicho ambaye ilikua haijatumika kwa muda mrefu,

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Mhandisi Adriano Nyaluke wakati alipokutanana Waandishi wa habari na kueleza mikakati ya kukiendeleza kiwanda hicho ikiwemo shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo ili baadaye kiweze kutoa ajira rasmi kwa Watanzania.

MhandIsi Nyaluke amesema kwamba, kwa sasa katika amamu ya kwanza wana mahitaji ambayo yanahitajika kukamilika ikiwemo mpango wa kutafuta fedha toka katika Mifuko ya Jamii ili kuweza kujenga mtambo huo pamoja na fedha za mtaji wa kutengeneza zana mbalimbali kiwandani hapo.

“Mpaka sasa tuna bajeti ya shilingi bilioni 1.6 na tuna mpango wa kuendelea kutafuta fedha zaidi toka katika Mifuko ya Kijamii na tunaamini fedha hizo tutazipata ili tuweze kuendelea na mpango wa kujenga mtambo huo pamoja na utengenezaji wa zana za kiwanda”, alisema Nyaluke. 
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), Mhandisi Adriano Nyaluke akiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya mitambo itumikayo kutengeneza vipuri mbalimbali vya mashine 13 Mei, 2017 Moshi, Kilimanjaro. 
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), Mhandisi Adriano Nyaluke (kushoto) akiwaonyesha Waandishi wa habari mashine ya kutengeneza randa zitumikazo katika kazi za useremala, 13 Mei, 2017 Moshi, Kilimanjaro. 
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), wakiwa kazini Moshi, Kilimanjaro 13 Mei, 2017. 
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Bw. Abel Ngapemba akiangalia moja ya mashine itumikayo kuchonga chuma wakati alipotembelea katika Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), kilichopo Moshi, Kilimanjaro 13 Mei, 2017. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...