Na Bashir
Yakub.
SHERIA ZILIZOPITIWA :
1. Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai,
Sura ya 20.
2. Sheria ya Huduma za Mashtaka
kwa Taifa, Na. 27/2008.
3. Kanuni
za Adhabu, Sura ya 16.
_______________
Tundu Lissu anasema anaamua
kumshitaki Makonda kwa kosa la kughushi nk. kwa kuwa Serikali imekataa na
haioneshi nia ya kumfikisha mahakamani Makonda.
Kama sababu ni kuwa serikali imekataa
kumpeleka Makonda mahakamani ndio maana Tundu Lissu na wenzake
wanaamua sasa kuchukua hatua basi nao hawatafanikiwa.
Kwa sheria ilivyo hawatafanikiwa mpaka
serikali wanayosema haitaki itake. Kwa mujibu wa kifungu cha
97 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kazi ya kufungua na kuendesha
mashtaka yote ya jinai ni kazi ya serikali kupitia ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).
Hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha
99(1) cha sheria hiyohiyo ni kweli bila ubishi kuwa mtu binafsi au Wakili
yeyote binafsi kama alivyo Tundu Lissu naye anaweza kufungua na
kuendesha mashtaka ya jinai dhidi ya mtu yeyote mkosaji kama ilivyo kwa DPP wa
serikali.
Pamoja na hayo kifungu cha 97 cha
sheria hiyo ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinasema kuwa ikiwa mashtaka
yamefunguliwa na mtu binafsi au Wakili binafsi kama alivyo Tundu Lissu basi
mwendesha mashtaka wa serikali akiamua anaweza kuchukua kesi hiyo.
Pia kifungu kinasema zaidi kuwa Wakili
huyo binafsi katika kesi hiyo aliyofungua atalazimika kufuata maelekezo
ya mwendesha mashtaka huyo wa serikali wakati wote wa
kesi.
Maana yake ni kuwa ikiwa mwendesha
mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kubadili jambo lolote katika kesi
aliyofungua basi atalazimika kulibadilisha. Lakini kubwa kuliko yote ikiwa
mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kufuta kabisa kesi ya
Makonda basi atalazimika kuifuta. Hii ndio maana ya kifungu hicho.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...