THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Kwese TV yawaunganisha wateja wa Vodacom kimichezo na burudani

Dar Es Salaam, 3 May 2017 –Wateja wa Vodacom Tanzania PLC – mtandao wenye kasi zaidi Tanzania, kuanzia sasa watafurahia kuona picha bora za video za michezo na burudani kupitia simu zao za mkononi kwa ushirikiano na Kwesé TV ambapo wateja  wataweza kuangalia picha za video mbalimbali kupitia TV ya mtandaoni ya Kwesé kwa gharama nafuu ya vifurushi vya data. 
Picha za video za Kwesé TV kwa njia ya simu zitaonekana kupitia program maalumu ya simu ya  Kwesé TV ambayo imesheheni video za michezo na burudani mbalimbali duniani ikiwemo mechi za Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza,mechi za ligi ya mchezo wa kikapu ya NBA,mashindano ya kimataifa ya mieleka na riadha ikiwemo picha za sinema na michezo ya kuigiza kupitia luninga.Burudani zote hizo zitapatikana kupitia mtandao wa Vodacom kupitia vifurishi vyake vinavyowezesha kupakua picha za video mitandaoni kwa gharama nafuu. 
Akiongea juu ya huduma hii mpya,Afisa Mtendaji Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, Ashutosh Tiwary alisema “Tunafurahi kushirikiana na luninga ya mtandaoni ya Kwesé kuwezesha wateja wetu kupata burudani ya picha za video wazipendazo kwa gharama nafuu ,huduma hii inadhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kubadilisha maisha ya watanzania kupitia ubunifu wa kiteknolojia na tuna imani watafurahia kutumia program hii kupakua na kuangalia video kupitia internet yetu ya kasi kubwa na wateja wanaotumia mtandao wetu wa 4G.” 
Kwa upande wake Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Econet Media inayomiliki televisheni ya mtandaoni ya Kwesé alisema “Tunafurahi kushirikiana na Vodacom Tanzania na tuna imani watanzania wengi wataweza kuangalia michezo na burudani mbalimbali zinazopatikana kwenye luninga yetu kupitia mtandao huu hususani katika kipindi hiki ambacho tumelenga kujiimarisha katika soko la Tanzania” 

Kwa maelezo zaidi kuhusu kupata huduma ya Progamu ya Kwesé  kupitia Vodacom tembelea tovuti yawww.Kwesé.com