Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Singida limeanzisha zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.

Amesema lengo ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.

Amesema pia wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani. 


Aidha RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si kuchangia kiti.

“Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.

Askari wa usalama barabarani mkoani Singida, E.8763. Sgt. Benes Lucas akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana. 
Baadhi ya mabasi kati ya 20 yanayotumika kusafirisha wanafunzi Mkoani Singida yakifanyiwa ugazi na askari usalama barabarani kwa lengo la kujiridhisha ubora wake. 
RTO Mkoa wa Singida Mrakibu wa polisi Peter Raphael Majira akitoa taarifa ya zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi kwa lengo la kukagua ubora na pia kuwakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo juu ya sheria za usalama barabarani. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...