THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKALA YA SHERIA: UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI KUREJESHA HASARA TULIYOIPATA HUU HAPA.

Na  Bashir   Yakub  
Mikataba yote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation). 
Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi  ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini  yapo kwa asili au yapo kwa kuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika katika mkataba. 
Mathalan, mfanyakazi  wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha  uaminifu  ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe  bado lipo tu.Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni  ya madini masharti yafuatayo ni ya  asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :

1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu  shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter). 
2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda  kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing). 
3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa  mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud). 
Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri  yake ni kukiuka masharti ya mkataba.

Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu  na masharti ya mkataba jambo ambalo  ni kinyume cha sheria. Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo  basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo.