THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Jukwaa la Dunia la Uchumi nchini Jordan


Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejenga uwezo zaidi wa kukabiliana na vitendo vya rushwa katika azma yake ya kujenga uchumi imara utakaostawisha Taifa kwa kuongeza Mapato kupitia Sekta ya Utalii sambamba na Ujenzi wa Viwanda vipya vya kudumu. 
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa la Dunia la Uchumi { world Economy Forum } wakati akiwasilisha Muelekeo wa Tanzania katika uimarishaji wa Sekta ya Utalii hapo katika Ukumbi wa Mfamle Hassan Bin Talal pembezoni mwa Bahari Nyeusi Mjini Amma Nchini Jordan. 
Balozi Seif alisema zipo jitihada za ziada zilizochukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ndani ya Sekta ya Utalii kutokana na Rasilmali nyingi zilizopo ikiwemo Mbuga za Wanyama, Ardhi yenye Rutba, Fukwe za kuvutia pamoja na Mlima wa Pili kwa urefu Duniani Kilimanjaro zilizoifanya Tanzania kujikita zaidi katika uimarishaji wa Seklta hiyo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tamasha la Uchumi la Dunia linalofanyika Mjini Amman Nchini Jordan akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.