Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017. Bajeti ya wizara hiyo imepitishwa jioni hii.
 Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Florens Turuka na Naibu Katibu Mkuu Imaculate Ngwalle,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo,Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa na Meja Jenerali Michael Isamuhyo wa JKT wakiwa katika kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Michael Isamuhyo katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa wakizungumza jambo na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama leo katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...