Michezo ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari-UMISSETA Copa Coca- Cola kwa Mkoa wa Mbeya imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sokoine na uzinduzi huo ulionogeshwa na wachezaji wa timu ya soka ya Mbeya City ambao walishiriki kufanya mazoezi na timu za wanafunzi na kutoa ushuhuda wa michezo hiyo ilivyoibua vipaji vyao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla,ambaye alikuwa mgeni rasmi anataka kuwaona vijana wengi wakishiriki mazoezi na michezo mbalimbali kwa kuwa michezo kama ilivyo hii ya UMISSETA Inaibua na kukuza vipaji pia sekta ya michezo bado inazo fursa nyingi za kujiajiri. 

Alisema kampuni ya Coca- Cola imeonyesha njia kwa kudhamini michezo hii na kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini michezo ya vijana kwa kuwa ndio tanuru la kuwaandaa wachezaji na kuibua vipaji. ‘’Leo hii tunaona hawa vijana wa Mbeya City wapo hapa kutoa ushuhuda wao, wanapokea mpunga (mshahara) wa maana lakini chimbuko lao wametokea kwenye michezo hii ya Copa Coca- Cola. 

Naamini kupitia michezo hii Mbeya tutapata wachezaji wengi zaidi’.Alisema. Ofisa Msaidizi Masoko wa Coca- Cola Pamela Lugenge, alisema lengo la kampuni ya Coca Cola kuuungana na Serikali kupitia UMISSETA ni kuona wanaibua vipaji vingi vya vijana walioko shule za sekondari ambako wanaamini ndiko chimbuko la kupata timu ya taifa na klabu mbalimbali nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Meneja Masoko Msaidizi wa Coca-Cola,Pamela Lugenge,akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za shule zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA Copa Coca-Cola wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...