NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewaomba wadau wamichezo nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwakuwa ni michezo kama ilivyo michezo mingine.

Meya Mwita aliyasema hayo jiji hapa leo katika uzindua wa mashindano ya mchezo wa Drafti yaliyofanyika katika viwanja vya mwembe yanga, halmashauri ya Temeke.

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Meya wa jiji Mwita , yalihudhuriwa pia na Mbunge wa jimbo la Temeke Abdala Mtolea , Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Drafti ambapo jumla ya washiriki 64 walishiriki.

Meya Mwita alisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini umekuwa ukizaraulika na kuonekana kwamba wanaoshiriki mchezo huo niwatu ambao hawana kazi za kufanya.

Alisema wapo wadau wengi ambao wanatoa vipaumbele kwenye michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete na michezo mingine huku wakiusahau mchezo huo , jambo ambalo linaonyesha kuwatenga makundi ambayo wamejikita kwenye mchezo huo.

Alisema “ Niwaeleze tu kwamba, huu mchezo ni mchezo mzuri kama ilivyo michezo mingine, leo hii wanaocheza mchezo huu wanazaraulika na kuonekana kwamba niwatu ambao hawana kazi, wasiojua kujishugulisha, jambo ambalo sio kweli natamani mchezo huu ufahamika kama michezo mingine.

“ Kama kweli tukiunga mkono mchezo huu, ipo siku tutajenga majina yetu kupitia mchezo huu kama ilivyokuwa kwenye mpira wa miguu, mpira wa pete, na hata mataifa ya nje yakatuunga mkono kupitia huu mchezo” aliongeza.

Aidha Meya Mwita katika hatua nyingine alisema kwamba ataunga mkono chama cha mchezo huo ili waweze kukisajili na kutambulika rasmi.

Aliongeza kuwa katika mashindano mengine , baada ya kusajiliwa kwa chama hicho, yatakutanisha kila halmashauri iliyopo jijini hapa na hivyo kupata mshindi kutoka kwenye halmshauri husika.

“ Jiji lina halmashauri tano, nataka kwenye mashindano mengine ambayo tayari chama hiki kitakuwa kimesajiliwa , kila halmashauri itashiriki, na mshindi atapatikana kutoka kwenye halmashauri nasio mmoja mmoja kama ambavyo tumefanya leo, ila huu ni mwanzo.

Hata hivyo Meya Mwita ameahidi katika mashindano yajayo kugharimia nauri na chakula kwa wachezaji watakao shiriki mashindano hayo na kuwa himzi wachezaji hao kuuthamini mchezo huo.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Meya wa jiji , Mwenyeiti wa Chama cha mchezo wa huo mkoa wa Dar es salaam , Kiraba Ngibombi amesema chama kinakabiliwa na changamo nyingi ikiwemo ukosefu wa ofisi na fedha za kuhudumia na kufanya usajili wa chama hicho.

Mwenyekiti huyo amemuomba Mstahiki Meya katika mashindano yajayo kuwagharimia wachezaji chakula na pamoja na nauri kwa ajili ya wachezaji hao.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdala Mtolea akicheza mchezo wa Drafti na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...