Na Tiganya Vincent, RS- Tabora
31 Mei, 2017
Jumla ya shilingi milioni 180
zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi huo
kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waindeshaji wa vyombo vya moto.
Takwimu hizo zilitolewa jana
mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano
na waandishi wa habari ofisi kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada
mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.
Alisema makusanyo hayo
yametokana tozo kwa madreva wa magari, pikipiki na bajaji na waendesha baiskeli
walivunjia Sheria za Usalama barabarani katika kipindi hicho.
Kamanda alitaja baadhi ya makosa
ni madereva wa Bodaboda kutovaa kofia ngumu wao na abiria wao , madereva wa
magari kuendesha bila kuwa na leseni, mwendokasi, kutozingatia alama za
barabara na kupakia abiria zaidi ya uwezo wa chombo cha usafiri.
Kamanda Mtafungwa alitoa wito
kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto Mkoani Tabora kuepuka kuvunja Sheria
za Usalama Barabarani ili waokoe fedha wanazozipata zitumike kusaidia familia zao
katika matumizi mengine ya maendeleo
badala kulipa faini.
“Naomba waendeshaji wa vyombo
vya moto kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ili wasipigwe faini ambazo
zinawafanya watoe fedha ambazo zingewesaidia wao na familia katika shughuli
mbalimbali” alisema Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...