· Mnufaika wa Airtel FURSA bidhaa zake ziko sokoni mikoa zaidi ya mitano

Mradi wa Airtel Fursa umeendelea kufanikiwa kwa kuendelea kuwezesha vijana nchini ambapo mmoja kati ya waliowezeshwa mwaka jana Bi Threria Maliatabu mkazi wa Mbagala jijini Dar es Saalam ameelezea jinsi mradi huo ulivyomuwezesha kukuza kipato na kupata mafanikio ya kuanza kujenga nyumba yake binafsi, kujinunulia shamba la eka 2 huku akiwaasa vijana wenzake nchni na wale wote waliowezeshwa na Airtel FURSA kuchangamkia fursa hizi pindi zinapotokea.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es saalam , Bi Maliatabu ambaye anajishughulisha na biashara ya uchoraji wa picha za sanaa alisema “ najivunia sana kuwa mmoja kati ya vijana walioshikwa mkono na Airtel Fursa kwa sababu program hii imeweza kunitoa kutoka niliopokuwa hadi kufika kwenye haya mafanikio niliyo nayo leo. 

 Kwakweli nimekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuboresha kiwango cha bidhaa zangu , nimefanikiwa kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba vinne na pia nimeweza kukunua shamba la eka 2 Mkuranga mkoa wa pwani. lengo langu ni kuanzisha shughuli za kilimo ili kutanua wigo wa biashara yangu lakini pia kuendelea na shughuli yangu ya uchoraji nayoifanya kwa sasa”

Aidha Maliatabu alifafanua kuhusu changamoto mbalimbali katika biashara ikiwemo masoko ya nje , usafiri wa kusambaza bidhaa zake huku akieleza kuwa baadhi ya changamoto hizi ameshaanza kuzishughulikia na kuomba wadau mbalimbali kuweza kumsaidia.
Theresia Maliatabu, mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa akimsikiliza mteja wakati alipohudhuria maonyesho ya bidhaa na kuonyesha kazi ya uchoraji wa picha za Sanaa anazozifanya hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...