WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wao wa jijini Arusha, Leopard Mpande, aliyetangazwa mshindi katika droo ya tisa iliyofanyika Jumapili, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema Mpenda ni mshindi akitokea jijini Arusha, baada ya kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko.

Alisema wanajisikia faraja kubwa kuona watu wanaingia kwa wingi kucheza mchezo wao wa kubahatisha na kuzoa mamilioni ambapo zaidi ya Watanzania 35,000 wameshinda zawadi mbalimbali.

Mgeta anasema hadi sasa wameshafanya droo kubwa tisa huku washindi wote wakiwa wameshakabidhiwa fedha zao hivyo kufanya jumla ya Sh Milioni 90 kuwafikia washindi wa droo kubwa za Sh Milioni 10.

“Huku Jumatano ya kesho tukitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wetu wa droo kubwa, tunajivunia kuona idadi ya wanaovuna mamilioni kutoka Biko inaongezeka kwa kucheza kwa kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo jinsi ya kucheza ni kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ikiwa ni 2456.

“Mtu anaweza kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi huku kila tiketi moja inayopatikana kwa Sh 1000 ikiwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, huku kwa Jumatano hii dau likipanda hadi Sh Milioni 20,” alisema Mgeta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania Charles Mgeta mwenye miwani akishuhudia katika makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wao wa jijini Arusha Leopard Mpande aliyepatikana katika droo ya Jumapili iliyopita. Aliyeshikana mikono na Mpande ni Balozi wa Biko Kajala Masanja.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko jijini Arusha, Leopard Mpande wa tatu kutoka kushoto akipokea nyaraka na fedha zake baada ya kukabidhiwa kutokana na ushindi wa droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumapili. Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Msanii Mpoki na maofisa wa NMB jijini Arusha.
Mshindi wa Biko jijini Arusha akisikiliza ushauri wa kifedha kutoka kwa afisa wa NMB Jijini Arusha jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...