Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo,amesema hakuna mtu anayeweza kukinunua Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa ni Chama kikubwa kilichoanzishwa na waasisi makini.

Amesema waasisi walizingatia misingi ya haki umoja na mshikamano ,wakaondoa dhulma, chuki na ubaguzi wa kila aina hivyo si rahisi mtu kufanya biashara na CCM.

Mpogolo alisema hayo jana alipozungumza na viongozi na wanachama wa CCM katika majimbo ya Temeke na Mbagala jijini Dar es Salaam,ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha Chama.

Alisema CCM inaendesha shughuli zake kwa uhuru na itahakikisha uchaguzi wake unafanyika kwa haki pasipo kuingilia na wanachama wenye tabia ya kununua madaraka.

Mpogolo aliwaagiza watendaji wa Chama na jumuiya kusimamia uchaguzi unaendelea kufanyika kwa haki bila kuwashinikiza wanachama kwa kuwa wanawafahamu viongozi wanaowataka.

"Hatutaki vurugu CCM, tunapenda amani,umoja na mshikamano. Wenye ni ya kutumia uchaguzi huu kupanga mitandao yao, wataambulia patupu,watatumia fedha na uongozi hawatapata,"alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana
Baadhi ya Wanachama wa CCM Kata ya Mtoni wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza kutoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala (hawapo pichani) kwa mapokezi, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwa Jimbo la Temeke jana.
Naibu akiagana na baadhi ya Viongozi ofisini kwa Mkuu wa Wilaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...