Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani Kibiti, Alife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha.
Kamanda Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo (Jumapili) katika Kijiji cha Nyambunda. Amesema Mtulia aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga.
Kamanda amesema mwili wa marehemu umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi.
Mauaji ya askari Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa yakifanyika mara kwa mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.
Jumanne wiki hii akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Mafia ili kuimarisha ulinzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...