THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Waziri wa nyumba ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema ataendelea kuwachukulia hatua wale wote ambao watakwenda kinyume cha sheria katika umiliki wa ardhi hapa nchini. 
 Mhe. Lukuvi alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu hoja za baadhi ya wajumbe wakati wa mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ambao walizungumzia changamoto kadhaa katika sekta ya ardhi. 
 “Kuna tatizo sana katika umiliki wa ardhi yetu, hasa haya mashamba makubwa, maana kuna baadhi ya watu wamechukua mashamba makubwa na kwenda kukopa katika mabenki na ukija katika hayo mashamba hakuna ambacho kimewekwa shambani kulingana na mikopo yao.
"Hivyo sasa sitasita kumchukulia hatua mtu yoyote ambaye atakwenda kinyume na na sheria za ardhi kwa kumnyang’anya hati yake na kuirudisha serikalini” amesema Waziri Lukuvi. Mhe. Lukuvi.
Pia ameweka wazi kuwa yupo radhi kutoa ardhi yenye hati ndani ya siku moja kwa mtu yoyote anayetaka kuwekeza viwanda hapa nchini na sio wababaishaji ambao wamegeuza ardhi kama mtaji wa kununulia mabasi kwa kukopa kwenye mabenki. 
Mhe. Lukuvi alimalizia kwa kusema kwa sasa wizara yake imeandaa vitabu ambavyo vinaonyesha watu wote wale ambao wanamiliki ardhi bila ya kufanya shughuli yoyote .

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi akizungumza na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania  Profesa Beno Ndulu
wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam Jumamosi.