TFS, Dar es Salaam.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Mamlaka ya Usafirishaji nchi kavu na Majini (SUMATRA) unazishikilia pikipiki 46 na baiskeli 30 kwa kosa la kusafirisha mazao ya misitu kinyume cha sheria ya misitu na kuwa na mazao hayo yaliyopatikana kinyume cha sheria.

Pikipiki na baiskeli hizo zilikamatwa kwa nyakati tofauti katika barabara kuu zinazoingia jijini Dar es Salaam kupitia Barabara ya Bagamoyo, Kilwa, Kisarawe na Morogoro.

Pikipiki na baiskeli hizo zilizokamatwa zitatozwa faini, pikipiki moja itatozwa faini ya kuanzia sh. 500,000/= huku baiskeli zikitozwa faini isiyopungua sh.50,000/= nakuendelea.

Faini hizi ni kwa mujibu wa Sheria ya Misitu inayoeleza wazi kuwa mtu yeyote aliyetenda kosa la kusafirisha mazao ya misitu yaliyopatikana kinyume cha sheria na kupatikana na hatia atatakiwa kulipa faini isiyozidi shilingi milioni moja au mara tatu ya thamani ya mazao ya misitu yaliyokamatwa au kifungo kisichozidi miaka saba au adhabu zote kwa pamoja.

Katika muda wa wiki mbili wa zoezi hilo jijini Dar es Dar es Salaam jumla ya sh. 11,167,600/= ilitozwa kama gharama za ufifilishaji (compounding fees) kwa magari yaliyokutwa na mazao ya misitu kinyume na sheria ya misitu na kanuni zake. Aidha gari moja lipo ofisi ya meneja wilaya ya bagamoyo kwa hatua Zaidi.

Pikipiki na baiskeli zilizokamatwa zimehifadhiwa katika ofisi ya Meneja Misitu Wilaya ya Temeke, Bagamoyo na Kibaha huku magunia 451 ya mkaa ambayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya takribani sh milioni 10 yakishushwa kutoka katika pikipiki hizo na magari yaliyokaguliwa.

Mkaa uliokamatwa umehifadhiwa katika ofisi ya Meneja Misitu wa Wilaya ya Mkurunga kituo cha ukaguzi cha Vikindu na ofisi ya Meneja Misitu wa Wilaya ya Ilala.

Ukaguzi wa kudhibiti vyombo vinavyosafirsha mazao ya msitu kinyume na sheria hususani baiskeli na pikipiki nchini ulianza Aprili 14 na zoezi hilo linalofanyika usiku na mchana ni endelevu hivyo wasafirishaji wa Mazao ya Misitu wanashauriwa kufuata taratibu na sheria za Usafirishaji wa mazao ya Misitu kwani kinyume na hapo adhabu husika itatolewa.


Tulizo kilaga

Afisa Habari na Mawasiliano
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) 03 Mei 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...