Mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo amewataka Watumishi katika sekta za umma kuacha dhana ya kuogopa kustaafu kazi pindi wanapofikia muda wa kustaafu badala yake wanatakiwa kujipanga kabla muda haujafika.

Aidha watumishi wanaogopa kustaafu kwa kuwa wanaanza kujiandaa miaka miwili kabla hali ambayo inawapa uoga mkubwa wastaafu watarajiwa.

Mrisho Gambo ameyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) uliokuwa ukiendelea jijini Arusha.

Gambo alisema kuwa kwa sasa wastaafu wanapata magonjwa ya moyo kwa kuwa hawajajiandaa na kubuni miradi ambayo inaweza kuwaletea vipato kama mishahara yao ilivyokuwa.

Alisema maandalizi ni muimu sana kwa wafanyakazi hata kama bado hawajafikia muda wa kustaafu kwani kustaafu sio ajali bali ni kitu ambacho kipo na kimeshawekewa utaratibu na mifuko ya hifadhi jamii hapa nchini pamoja na Serikali.

"Wastaafu wengi wanakufa pindi wanapoacha kazi hiyo sio sawa ni lazima kila mtu ajiandae na abuni njia mojawapo ya kujiongezea kipato kwani hata kama ukijiajiri mwenyewe ni lazima utapata kipato kama kile ulicho kuwa unalipwa kama sehemu ya ujira wako "aliongeza Gambo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF jijini Arusha juzi ,wakati akifunga mkutano huo ambapo aliwataka wastaafu watarajiwa kujiandaa kustaafu kwa kubuni miradi mbalimbali ya kuongeza kipato hali itakayosaidia wao kujiendeleza kimaisha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema ni vyema watumishi wakajianda mapema wakiwemo wa umma na sekta binafsi .
Mkurugenzi wa mfuko wa GEPF Daudi Msangi alisema kuwa tayari kuna mikakati mbalimbali ambayo imeletwa kwenye mkutano huo na itaanza kufanyiwa kazi kwa malengo ya kuboresha maslai ya wanachama na nchi kwa ujumla.

Wadau wa mkutano wakiwa wamesimama kuashiria kumalizika kwa mkutano huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...