Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema
kuwa timu ya Taifa Stars itafanya vizuri katika mashindano mbalimbali
itakayoyakabili hapo baadae,kutokana na wadau wanavyojitokeza kuiunga
mkono.
Mwakyembe
ameyasema hayo wakati kishuhudia utiaji saini mkataba kati kampuni ya
ya Bia ya Serengeti (SBL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF)
wenye thamani ya sh.bilioni 2.1,utakaodumu kwa miaka mitatu na kuifanya
SBL kuwa mdhamini mkuu wa timu ya Taifa Stars.
“Kwa
niaba ya serikali,tunaishukuru sana kampuni ya SBL kwa kurejea tna kuwa
mdhamini mkuu wa Taifa Stars,lakini pia tunatoa wito kwa kampuni
zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa
michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo hapa nchini”,aliesema
Waziri Mwakyembe.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL ,Helene Weesie amesema kuwa SBL imekuwa
mdhamini kwa kipindi cha pili baada ya kampuni hiyo kufanya udhamini wa
timu ya taifa stars mwaka 2007 hadi 2011.
Amesema
timu ya Taifa Stars itakuwa inapokea sh.milioni 700 kila mwaka ambapo
itakuwa ni pamoja na kutangaza chapa ya SBL wakati wa mechi za ndani na
ugenini zitakazochezwa na timu hiyo.
Kwa
upande wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameishukuru SBL kwa kuunga mkono
katika kusaidia maandalizi ya timu ya taifa Stars,akaongeza kusema kuwa
udhamini huo utasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki
kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani na nje ya
nchi.
“Udhamini
wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo
katika hatua za maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,”
alisema Malinzi.
Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia ) akipeana mkono na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) mara baada ya kukabidhiana
mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1,Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) kwa pamoja wakionesha mikataba waliowekeana saini, leo mbele ya Waandishi wa habari,kwenye hafla fupi iliofanyika jioni ya leo jijini Dar.Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Pichani kati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jioni,kwenye hafla fupi ya uwekaji saini mkataba kati ya kampuni ya ya Bia ya Serengeti (SBL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wenye thamani ya sh.bilioni 2.1 .
Baadhi ya Waandishi wa Habari na baadhi ya wafanyakazi wa TFF na Wizara wakishuhudi tukio la uwekaji saini mkataba wa udhamini kwa timu ya Taifa Stars wenye thamani ya sh.bilioni 2.1 uliotolewa na kampuni ya SBL na hatimaye kuifanya kampuni hiyo kuwa mdhamini mkuu wa timu ya Taifa Stars,hafla hiyo imefanyika jioni ya ya leo jijini. Picha na Michuzi Jr.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...