Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali imesema kuwa haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akijibu hoja mbalimbali  Mjini Dodoma.

“Kutokana na faida na Mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali inaamini kuwa zipo faida nyingi ndani yake na mwenge huu utaendelea kudumu”,Alisisitiza Mhe.Muhagama.

Amesema kuwa Kimataifa Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Afrika na Dunia kote.

Aidha amesisitiza kuwa Umoja ,Mshikamano ,Upendo na Ukarimu wa Watanzania  ni matunda ya Mwenge wa Uhuru.

Mhe.Muhagama ametoa takwimu ambazo zinaonyesha kuwa Miradi ya Maendeleo iliyozinduliwa pamoja na kuwekewa mawe ya msingi kupitia Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2015 ni miradi 1342 yenye thamani ya bilioni 463,519,966,467.

Pamoja na hayo amezitaja faida za Mwenge wa Uhuru kuwa ni kuendelea kuamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu,pia kimekuwa ni chombo pekee cha kujenga umoja na mshikamano na kudumisha amani pale unapopita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa.

Aidha Mwenge wa Uhuru umeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa pande mbili za nchi yetu na kila mwaka huweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi na kuhamasisha uzalendo wa kuendelea kujitolea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...