SERIKALI yaja na mpango mkakati wa kudumisha matibabu ya uzazi pingamizi ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini Tanzania. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati waa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika jijini Dar es salaam. 

“Huwezi kutoa huduma bora na salama ya uzazi pingamizi bila kuwa na wataalamu wa ganzi ili kufanywa upasuaji usio na maumivu hivyo katika mkutano huu tunapanga kuwa na wataalamu wengi wa huduma hiyo ili kutoa huduma bora nchini. 

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa licha ya kudumisha matbabu ya uzazi pingamizi pia Serikali imejidhatiti kujenga vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla. 

Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mkutano huo unalenga kutoka na malengo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa mahututi pamoja na kutoa huduma ya ganzi kwa wanaohitaji kupasuliwa. Mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha Wataalam Wa Ganzi nchini (SATA) umeudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Sweden,Cameroon, Marekani , Tanzania ili kuweza kujua mchango wa kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na huduma ya ganzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakimsikilliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...