Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina kwa Viongozi wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.

Semina hiyo ya siku tatu, kuanzia jana Mei 09 imewashirikisha Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na kulinda maslahi ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na utumikishwaji wa kazi ngumu na maslahi duni.

Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina hiyo ambapo pia ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao kuitambua Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu ya umri huo wakipaswa kuajiriwa kufanya kazi zisizo hatarishi.

Aidha amekumbusha juu ya kuutambua Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 ambao unaelekeza kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...