THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TADB YATEMBELEA VYAMA VYA USHIRIKA VYA MSINGI MANYARA

Na Mwandishi wetu, Manyara
Katika kufanikisha azma yake ya kuwa benki kiongozi  katika kuleta maendeleo ya kilimo nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imevitembelea vya ushirika vya msingi mkoani Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.

Akizungumza wakati wa ziara zake katika vijiji vya Masakta, Gallapo na Gendi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki yake ina Dira ya kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Hivyo TADB ina wajibu wa kuwasaidia wakulima nchini ili kuwafikisha katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Bw. Assenga aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwanyanyua wakulima katika uongezaji tija wa kilimo nchini kwa kutoa mikopo na kusaidia shughuli mbali mbali za uongezaji tija katika kilimo.

“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima TADB kwa kushirikisha wadau wa Kilimo, utafiti na huduma za ugani tumejipanga kuwapatia wakulima mafunzo ya kilimo cha kisasa cha ili waweze kutumia mbinu bora za kilimo,” alisema.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Homari AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
 Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akitaja fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya Kilimo wakati wa kikao cha pamoja kati ya TADB na Bodi ya Homari AMCOS wakati walipotembea vya ushirika vya msingi vya mkoa wa Manyara ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza mkoani humo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Homari AMCOS iliyopo katika Kijiji cha Masakta, Bibi Magreth Mgeni (kushoto) wakikagua mahindi katika moja ya mashamba waliyoyatembelea.
 Sehemu ya mahindi yaliyokwisha vunwa yakiwa yamehifadhiwa Kijijini Masakta.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA