Uandikishaji
ulifanyika Tegeta Complex jijini Dar es Salaam huku timu zaidi ya 20
zikijitokeza kujiandikisha. Michuani ya Sprite Bball Kings inaendeshwa
na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa
udhamini wakampuni ya Coca-Cola.
Ikiwa
ni siku ya kwanza kwa timu mbali mbali za michuani ya kikapu ya Bball
Kings, zaidi ya timu 20 zimejitokeza kujiandikisha mwishoni mwa wiki hii
wakati wa zoezi la uandikishaji linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Michuani
ya mchezo wa kikapu ya Bball Kings inayoendeshwa na kituo cha
Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa kushirikiana na
Kampuni ya Coca-Cola kupitia kinywaji chake cha Sprite siku ya jumamosi
imeshuhudia wawakilishi wa timu mbalimbali wakijitokeza na kujaza fomu
za ushiriki, huku wawakilishi wa timu hizo wakijigamba kujidhatiti
kikamilifu kuchukua ubingwa wa mwaka huu.
Kati
ya timu zilizojitokeza ni pamoja na Cavarious, Lycans, Tegeta Camp,
Lord Baden, K-Warriors, DMI, St Joseph na MJ Junior.
Nyingine ni Oilers, TMT, Mchenga, Bahari Beach, Street Boys, Street
Warriors, Chanika Legends, God With Us, Weusi Basketball Club, Junior
Basketball Club na Celestial Basketball Team.
Akizungumza
wakati wa uandikishaji wa timu shiriki, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na
Masoko wa wa EATV, Roy Mbowe alisema mwitikio wa timu mbalimbali umejaa
hamasa kubwa na wa kuridhisha, huku kila timu iliyojitokeza ikiwa na
wachezaji wasiozidi 10.
“Mashindano
hayo yanahusu vijana wenye umri wa kuanzia miaka 16 na watapaswa kuunda
timu ya wachezaji 10 ambao watachuana na timu nyingine zitakazokuwa
zimejiandikisha, huku tukitoa fursa katika wachezaji hao 10, timu
inaweza kuwa na wachezaji wasiozidi watatu kutoka katika timu kubwa za
Ligi Darasa la Kwanza za za kikapu za hapa nchini,’’alisema Mbowe.
Michuano
ya Sprite Bball Kings itaendeshwa kwa njia ya mtoano katika hatua ya
kwanza ili kupata timu 16 zitakazoingia hatua ya pili na kutaja zawadi
kwa timu itakayotwaa ubingwa itakuwa ni Sh.milioni 10 wakati mshindi wa
pili atapata Sh.milioni tatu huku pia kukiwa na zawadi ya Sh milioni
mbili kwa mchezaji bora (MVP).
Mashindano hayo yatakayoshirikisha wachezaji kutoka mikoa yote nchini,
yanatarajiwa kuanza mwezi huu na kumalizika Julai mwanzoni.
Kiongozi wa timu ya mpira wa kikapu ya Weusi Basketball Club ya jijini Dar es Salaam, Mntambo Mngeja (kulia) akipata maelekezo ya juu ya kujiandikisha kutoka kwa mratibu ya michuano ya Sprite Bball Kings, Basilisa Biseko wakati wa zoezi la uandikishaji wa timu mbalimbali kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...