Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kivunjo, Ki-Old Moshi, Kiuru, Kikibosho, Kimachame, na Kisiha. 
Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Ki-Old Moshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. 
Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo. 
Usipate shida ndugu yangu. Ukitaka kujua mengi zaidi juu ya Wachagga, ama kupanda Mlima Kilimanjaro, ama kutembelea mbuga za wanyama za Kaskazini, tembelea MOSHI ambao unasifika nchini kuwa ni mji msafi kuliko yote. 
 Na unapokuwa hapo fikia EASTPOINT HOTTEL iliyopo kona ya mitaa ya Swahili na Liwali katikati ya mji wa Moshi. Ni hoteli mpya na ya kisasa inayoongoza kwa huduma bora na mandhari nzuri za Mlima Kilimanjaro.
Kwa maswali na taarifa zaidi kuhusu 
EASTPOINT HOTEL BOFYA HAPA
Mandhari mwanana ya mji wa Moshi na Mlima Kilimanjaro.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...