Na mwandishi wetu, Arusha

Wadau wa sekta ya mifugo mkoani Arusha wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza sekta hiyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa nyama na maziwa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, kwa niaba ya wafugaji wa mkoa wa Arusha, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi amesema ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika sekta ya mifugo inawapa changamoto katika uendelezaji wa sekta ya mifugo nchini.

Bw. Kissiagi ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika inarudisha nyuma ukuaji wa sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.

“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha kuhusu fursa za mikopo ya TADB. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...