Na Nuru Juma & Husna Saidi-Maelezo.

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linajiandaa kushiriki mashindano ya kanda ya Zone 5 Kimataifa kwa watoto chini ya umri wa miaka 16 yatakayofanyika mjini Mombasa nchini Kenya kuanzia tarehe 1-6 Juni mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es salaam leo, Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Michael Mwita alisema mashindano hayo yatatumika kupata timu  itakayowakilisha kanda ya Zone 5 na baadaye kuwakilisha  bara la Afrika katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo.

Alifafanua kuwa zimeundwa timu kutoka Mikoa mbali mbali ambapo mazoezi rasmi ya mchujo wa wachezaji kupata timu itakayowakilisha Taifa yataanza tarehe 20 mwezi  huu katika viwanja vya JMK sports Complex jijini Dar es Salaam.

“Tumeshathibitisha ushiriki wa timu yetu na vijana wameshaanza mazoezi tangu mwezi Januari na tumeandaa bajeti ya mil.30 ili kuweza kufanikisha mashindano hayo ambayo kwa Tanzania ni mara ya kwanza kushiriki”, alieleza Mwita.

Aliongeza kuwa mshindi atakaepatikana kwa kanda ya Zone 5 atakutana na washindi wengine wa kanda sita kwa upande wa bara la Afrika na kisha kupata timu itakayowakilisha bara la Afrika na kukutana na bara la Amerika, bara  la Ulaya na bara la Amerika ya Kusini ili kumpata mshindi wa Dunia.

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo, Bahati Mgunda alisema ameamua kuteua makocha wasaidizi katika Mikoa mbali mbali ili mchezo huo wa kikapu uweze kuenea nchi nzima.

Mgunda alisema wanahitaji kuwalea watoto wa jinsia zote wenye umri kuanzia miaka 11 hadi 14  watakaopenda kujiunga na mchezo huo wa mpira wa kikapu na baadaye kuwaunganisha katika timu kubwa na kuweza kushiriki mashindano ya Kitaifa.


Katika kanda ya Zone 5 nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Sudan, Sudani Kusini, Uganda, Burundi, Rwanda, Misri na Somalia. 
 Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Mwita akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuwaomba wadau kuichangia shilingi milioni 30 kwa timu ya Vijana U-16 wa mchezo ikiwa ni ghalama ya kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa kikapu chini ya umri wa miaka 16, Bahati Mgunda akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akielezea programu nzima ya maandalizi ya hiyo inayojiandaa kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...