Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ameiagiza Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kufanya tafiti kujua chanzo cha mmongonyoko wa maadili kwa wafanyakazi wa afya wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.

Alishauri baada ya kupata majibu ya tafiti hizo kuishauri serikali hatua ya kuchukuliwa ili kuinusuru hadhi ya taaluma ya afya ambayo inajengeka katika misingi ya ukarimu na kutoa huduma bila upendeleo.

Naibu Waziri ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku nne juu ya Maadili na Utafiti kwa wakufunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba na viongozi wa wauguzi wa Hospitali binafsi na Serikali katika skuli hiyo iliopo Mbweni.

Alisema watendaji wa Hospitali na vituo vya afya na hasa vya Serikali baadhi yao wanakiuka maadili ya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wagonjwa na kuwatolea lugha mbaya

Alisema tatizo la unyanyasaji wagonjwa limekuwa kubwa zaidi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo ni tegemeo kubwa la wananchi wa Zanaizbar.
Kaimu Naibu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Bi. Amina Abdulkadir akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kufungua warsha ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli hiyo na viongozi wa wauguzi wa Hospitali za Serikali na Binafsi huko Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akisisitiza maadili kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya wakati akifungua warsha ya siku nne ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi katika skuli hiyo iliopo Mbweni.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya maadili na utafiti wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo inayofanyika Skuli ya afya na Sayansi za tiba Mbweni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...