MAAFISA Afya toka kitengo cha magonjwa ya dharura mkoa wa Songwe wameweka kambi kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), ili kubaini abiria wenye dalili za ugonjwa wa Ebola ulioibuka hivi karibuni kwenye nchi ya jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Kiwanja cha Kimataifa cha Songwe kilichojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mwaka 2012 kinapokea abiria 500,000 kwa mwaka kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. TAA inahudumia viwanja 58 vilivyopo chini ya serikali.

Afisa Afya Bw. Peter Alfred amesema wamefunga mashine maalum na ya kisasa kiwanjani hapo, ambayo abiria akipita umbali wa mita tano hadi 10 inampiga picha na kuonesha joto alilonalo mwilini, na endapo atakuwa na joto la nyuzijoto 37.5 mashine hiyo itatoa mlio wa kengele.

Bw. Alfred amesema abiria atakayekuwa na joto hilo, atachukuliwa na kupelekwa eneo maalum lililotengwa umbali wa mita 300 kutoka eneo la kiwanja cha ndege na baadaye kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.
Afisa Afya Bw. Peter Alfred (katikati) akikagua hati ya kusafiria ya Bw. Paluku Ngahngondi (kushoto) Mkongo anayeishi Zambia, kabla ya kupanda ndege ya Fastjet kuja Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Afya Bi. Shukrani Nkonjeka akiwa kwenye mashine maalum inayompima kila abiria anayepita mbele yake kwa kupiga picha na kutoa mlio wa endapo anajoto kali la mwili.
Bi. Shukrani Nkonjeka, Afisa Afya akimpa maelezo kuhusiana na ugonjwa wa Ebola, mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), Bw. Fred Martin (kushoto).
Bi Shukrani Nkonjeka, Afisa Afya akiwapa maelezo yanayohusiana na ugonjwa hatari wa Ebola madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA).
Madereva wa taxi wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), wakipokea vipeperushi vyenye maelezo mbalimbali yanayohusu ugonjwa hatari wa ebola kutoka kwa Afisa Afya, Bi. Shukrani Nkonjeka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...