Na Ankal
Hebu jaribu kulielezea jiji la Dar, au la Arusha, ama la Mwanza,  Mbeya  ama jiji lolote lile, tena  kwa kutumia ukurasa mmoja tu na uwe umefanikiwa kulieleza kinagaubaga kiasi hata mtu ambaye hajawahi kufika hapo ajione kama keshafika na anapafahamu vizuri.

Basi huo ndio mtihani niliokumbana nao wakati najitahidi kuandika haya, kwa moyo mzito, nikijaribu kumwelezea rafiki yetu, kaka yetu, ndugu yetu, jamaa yetu au vyovyote vile upendavyo kumwita mtu kama Balozi Abdulcisco  Omar  Mtiro - almaarufu kwa jina la CISCO - ambaye leo adhuhuri tunampumzisha kwenye nyumba yake ya milele kwenye makburi ya Kisutu.
Labda uamue uzungumzie kamtaa kamoja tu katika kitongoji kimoja, ndio kidooooogo unaweza kufanikiwa kueleza vitu vikaeleweka - Nami ndivyo naitajaribu kufanya hapa,  kwa kudonyoa kasehemu kamoja tu ka Braza Cisco.

Ni kweli kwamba mtu akitangulia mbele ya haki huwa kuna hulka ya kumsifia na kumuenzi mtu huyo. Lakini si uwongo kwamba haya niandikayo hapa, japo yalikuwa nyuma ya ubongo wa wengi wetu siku zote, ni halisi na wala sio kwa sababu Cisco hatunaye tena.

Naam, kwa wengi alikuwa mkarimu na mwingi wa bashasha saa zote. Kwa tuliobahatika kuwa karibu naye, Cisco alikuwa hivyo na zaidi. Pamoja na kuwa na wadhifa mkubwa serikalini (Balozi wetu nchini Nigeria na Malaysia katika nyakati mbalimbali na baadaye Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje), Cisco alikuwa mtu wa kujichanganya na kila mtu bila kujali hali ama mali zake. Hakuwa na makuu wala makidai. Alikuwa mtu mmoja 'freshi' ile mbaya, wanasema vijana wa mjini.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...