MSHINDI wa Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ wa droo ya 13, Amani Kabuku, jana amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa zawadi hiyo ya donge nono itamkomboa kiuchumi, licha ya umri mdogo aliokuwa nao, akiwa na miaka 23 tu.

Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.

Alisema amecheza mara nne tu kabla ya kutangazwa mshindi katika droo ya 13 iliyofanyika Jumapili iliyopita, ambapo hata hivyo hakuamini haraka hadi alipowaona baadhi ya wafanyakazi wa Biko walipomfuata nyumbani kwao kwa ajili ya kumhakikishia juu ya ushindi huo.

“Ni furaha kubwa niliyokuwa nayo kwa sababu naamini huu ni wakati wa kuaga umasikini maana wengi wanatafuta nafasi kama hii ambayo leo Mungu ameniletea mimi ili niweze kutimiza ndoto zangu katika umri niliokuwa nao, hivyo nawashukuru Biko, huku nikiwataka Watanzania wacheze kwa wingi ili nao washinde kama ilivyokuwa mimi,”

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, akiwa katika furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.  


Mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 13 ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, katikati akiwa amepakatia fedha zake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyekamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mshindi huyo na kuingiza pesa zake. 

Akizungumza kwa furaha kubwa, mshindi huyo alisema ndio kwanza amemaliza kidato cha sita na kuibukia kwenye fedha hizo za Biko, hivyo anaamini zitamkomboa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maisha yake yanakuwa mazuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...