THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BALOZI MASIMA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA TAIFA LA ISRAEL


Kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kufungua ubalozi wa Tanzania jijini  Tel Aviv nchini Israel, na balozi mteule kuwasili kituoni, jana Alhamis tarehe 15 June 2017  Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Job Masima amewasilisha Hati za utambulisho kwa Mhe. Reuven Rivlin, Rais wa Taifa la Israel jijini Jerusalem. 
Katika sherehe hiyo, Rais Rivlin alimshukuru Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli, kwa kumteua balozi mkazi wa kwanza ubalozi nchini Israel . Ampongeza pia kwa hatua mbali mbali anazozichukua katika kukukuza uchumi na kusifia serikali yake kwa kudumisha hali ya utulivu na amani nchini Tanzania. Kwamba anaiona nchi  ya Tanzania ikiwa yenye maendeleo makubwa mbeleni chini ya uongozi wake. Kwa upande wake, pamoja na mambo mengine, balozi aliwasilisha salamu maalimu za Rais Magufuli kwa Rais Ruvlin, serikali na wananchi wa Israel na kuahidi kudumisha mahusiani yaliyopo na yenye historia kubwa. Ubalozi wa Tanzania umepewa usajili wa kibalozi namba 88.
 Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akipokewa kwa nyimbo za taifa baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akiweka saini kwenye kitabu maalumu cha wawakilishi wa nchi za nje kwenye Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin aliyesimama kulia kwake
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akijitambulisha kwa  Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho

 Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin  Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem 
  Akiwa amevaa baragashia ya kitamaduni ya Kiyahudi maarufu kama "Kippah" Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na kusoma salamu maalumu za mwanzo wa urafiki mpya wa ushirikiano wa karibu kwa ki-Hebrew baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin  Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa taarifa zaidi za hafla hiyo BOFYA HAPA