Baadhi yetu huwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....
Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi, mwili mfupi, utofauti wa tambo la kichwa,vidole vya mikono na miguu,nk.
Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini kwake, Ijumaa 16, Juni 2017.
Mbali na kuwanyanyapaa, jamii zetu Afrika bado hazitambui umuhimu wa kuendeleza wenye ulemavu.
Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio Ubongo “ (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa wa upigaji picha.
Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro akaeleza:
“Wametoka vijana wengi kwenye nchi zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku, picha yake imeshinda...”
Mwasisi wa kujitolea wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite na wazazi wake Samwel, Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo. Picha na Habari za Freddy Macha
Samwel Mwanyika na picha iliyonyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
Balozi Migiro, na Afisa Utawala Ubalozi London wakiwa na Samwel Mwanyika na mwenzake mwenye “Mtindio Ubongo” (Down Syndrome), Penina Haika Petitte.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...