THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Na.Vero Ignatus, Arusha.

 Baraza la Wazee Jijini Arusha wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwaangalia wazee ambao walikuwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki awalipe  stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii mambo mazuri bali manufaa wameyakosa baada ya kuvunjika Jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari  kwa niaba ya wazee hao mwenyekiti wa Baraza hilo  Mathius Kichao amesema  kuwa hadi sasa kuna wazee ambao hawajalipwa stahiki zao jambo ambalo siyo zuri hata kidogo kwani wazee hao wananung'unika

  "Kuna muda wazee hawa waliandamana wakenda Dar es salaam ,wakalala barabarani,lakini viongozi wawakati ule hawakuona umuhimu kuwa kilio cha wazee ni hatari sana wakawafukuzwa,nitamke kuwa hadi sasa kuna wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa chochote kile, niikumbushe Serikali wale wazee wanalaani ,naomba hii laana isitokee,Mhe,Magufuli awalipe stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii vizuri zaidi  "alisema Mwenyekiti huyo

 Aidha wazee hao  katika jiji la Arusha wameiomba serikali ya awamu ya tano ipeleke  mswada wa wazee katika Bunge la Jamhuri ya Muungano  na upitishwe  ili  Wazee nchini Tanzania  waweze kunufaika na matunda ya nchi yao kwani  wao ni chombo cha harakati hivyo Taifa likiwasahau wazee hakuna maendeleo kwasababu  wazee  huwa  wanafahamu mambo mengi ya kihistotia ya Nchi pamoja na mila nzuri na desturi.

"Tunawaomba viongozi mbalimbali wa Taifa hili wanapotembelea mkoa wa Arusha watenge muda wao ili waweze kuonana na wazee tutawashauri kwa yale tunayoyafahamu kwaajili ya manufaa ya nchi yetu na watoto pamoja na wajukuu zetu.
Mwenyekiti wa Baraza la wazee mkoa wa Arusha Mathius Kichao aliyeshika karatasi mkononi,akiwa anazungumza na waandishi wa habari hivi katibuni Jijini hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa wazee wa Baraza la wazee Jijini Arusha Kassim Seremuka  akizungumza jinsi ambavyo wazee hao wamenifaika na vitambulisho vya bima ya afya .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Baraza la wazee katika mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja .Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa Baraza la wazee Kassim Seremuka Jiji la Arusha akionyesha Kadi ya matibabu wanazotumia wazee wakienda kutibi wa Hospitalini.