THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Bendera ya CHADEMA Kupeperuka Nusu Mlingoti kuomboleza kifo cha Mzee Philemon Ndesamburo

Kufuatia kifo cha mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee Philemon Ndesamburo Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji, ametoa maelekezo kwa watendaji nchi nzima kupeperusha bendera nusu mlingoti.
Mashinji ametoa maelekezo hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam na kusema bendera zinapaswa kupeperushwa nusu mlingoti hadi mwili wa kiongozi huyo utakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.
"Chama kitashiriki katika msiba huu kwa heshima zote kumuenzi mmoja wa waasisi wa siasa za mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli nchini, msiba huu ni msiba wa CHADEMA, ni msiba wa Watanzania, ni msiba wa Taifa letu kutokana na mchango mkubwa wa Mzee wetu kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu, Mhe. Ndesamburo ndiye aliyekifadhili Chama kwa mara ya kwanza kwa kukipatia ofisi eneo la Kisutu jijini Dar es salaam" amesema Dkt. Mashinji