Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.

Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Hamphrey Pole Pole, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais Dkt Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa. 

Pole Pole amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi wa nchi. 

Pamoja na mambo mengine, Pole Pole, amesema kilichofanywa na Rais Magufuli ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini. 

Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na MmIliki wa Kampuni ya Acacia kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa na Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...