THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DAWASCO YATOA NOTISI KWA WADAIWA SUGU WA BILI ZA MAJI

Dawasco inawatangazia wateja wake wote wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, pamoja na Mji wa Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani wenye madeni ya bili za Maji kwa kipindi cha zaidi ya Mwezi mmoja kuwa, wanatakiwa kulipa madeni yao kabla ya tarehe 11.06.2017, kinyume na hapo Dawasco inakusudia kuwafikisha Mahakamani wateja wote wanaodaiwa kipindi hicho cha zaidi ya mwezi mmoja.

Taarifa hii inawahusu wateja wote wenye madeni pamoja na wale watakaoshindwa kulipa madeni yao ndani ya muda uliotajwa.

Mteja atakayeshindwa kulipa deni lake ndani ya muda tajwa atalazimika kulipia bili yake, pamoja na gharama zote za kuendesha kesi kwa wale watakaofikia hatua ya kufunguliwa mashtaka na faini.

Kumbuka Dawasco haipokei Malipo taslimu (Mkononi), malipo yote yafanyike kupitia huduma za Kibenki, mawakala wa Selcom na Maxcom, pamoja na mitandao yote ya simu ambayo imeidhinishwa.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba 0800110064 (BURE)

IMETOLEWA NA MKURUGENZI MKUU
DAWASCO