Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameiagiza Mamlaka ya mapato nchini TRA ngazi ya Wilaya ya Kinondoni kubadilisha mfumo wa ukusanyaji wa kodi ili kuongeza mapato ya serikali kutoka Bilioni 40 na kuendelea.
Hapi amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara la Wilaya ya Kinondoni katika hoteli ya Traventine Magomeni, amesema kuwa serikali ni lazima ikusanye kodi ambayo inatokana na wafanyabiashara.
Hapi amesema kuwa kufikia malengo ya zaidi ya ukusanyaji wa sh. bilioni 40 kwa kuwaingiza katika mfumo wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) kwa kuwa na vitambulisho maalum ili waweze kulipa kodi .
Amesema kuwa kuwaingiza machinga katika mfumo ndio utakuwa urasimishaji wa machinga hao kwa kuweza kukopesheka katika taasisi za fedha ikiwa ni pamoja kwa TRA kuweka vituo vya forodha katika Bandari Bubu za Mbweni ili kudhibiti mizigo inayoingia kinyemela kutokea visiwa Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya, Hapi Amesema kuwa kumekuwa na tatizo la uwepo wa leseni feki za biashara ambazo zinatolewa na watu feki nje ya ofisi za TRA na Manispaa ili waweze kukwepa kodi na kutafuta rekodi mpya ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakibuka kila siku katika Wilaya hiyo ambao wanastahili kulipa kodi kwa kuanza kupewa elimu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyabiashara Wilaya ya Kinondoni katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Traventine Magomeni.
Afisa Biashara wa Manispaa wa Manispaa ya Kinondoni, Mohamed
Nyasama akizungumza juu ya hali ya biashara katika Manispaa hiyo .
Sehemu Wajumbe wa Baraza la Wafanyabiashara la Wilaya ya Kinondoni katika mkutano uliofanyika katika Hotel ya Traventine Magomeni leo jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...