THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HIFADHI YA TAIFA MIKUMI MKOANI MOROGORO YAJIVUNIA IDADI KUBWA YA WAGENI

ikumi mkoani Morogoro ni moja ya mbuga za wanyama ambazo kwa sasa hujivunia idadi kubwa ya wageni na wanyama makundi tofauti wakiwemo simba pia ni hifadhi ambayo hufikika kwa urahisi na kuwafanya wageni kuona wanyama kwa haraka. 
Hifadhi imeshirikiana na vijiji katika kuunda ujirani mwema kupitia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi ili kuhakikisha maafisa wa wanyamapori wanashirikiana na wanavijiji kulinda mipaka ya hifadhi ya taifa mikumi dhidi ya ujangili. 
Mbuga ya wanyama Mikumi hupokea wageni wa aina mabalimbali wakimiwemo wenyeji wakazi kwa vingilio tofauti ukilinganisha na watalii wandani ambapo vingilio vyao ni shilling 5700 kwa mtu mzima.
 Muongozaji wa hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa mkoani Morogoro Yuston Bonike akimuonyesha muandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Ashton Baraigwa mbegu ya mimea ambayo inaweza kuliwa na nyani kipindi cha ukosefu wa chakula na kumletea madhara na nyani huyo kugeuka kuwa kichaa.
Moja wa maporomoko ya maji kivutio ambacho kina patikana katika hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambacho hufikiwa kirahisi kwa njia ya miguu na hupatikana ndani ya msitu huo.
Tembo nao ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi ya taifa Mikumi mkoani Morogoro ambao mara nyigi hupenda kutembea kwa makundi wakati wa kujitafutia malisho.
Kikundi cha utunzaji wa mazingira kinachotokana na mradi wa utalii wa kitamaduni wakiwa wameshikilia vikapu ambavyo vimetengenezwa na mifuniko ya chupa za maji ambayo wamekuwa wakiyaokota. Wa pili kutoka kulia ni katibu wa kikundi hicho Bw. Christandus Mdoe. Picha zaidi BOFYA HAPA