Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro juni 6 alifanya mazungumzo na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini wahalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.

IGP Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewahakikishia wananchi kuwa wahalifu wao ni lazima watapatikana.

“Kubwa ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa wahalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya,” alisema IGP Sirro na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba waendelee kukimbia lakini njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku tutawarudisha kwenye mstari"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...